Spiritual Healing
Kuogopa wakati wa usingizi, kulia sana, kupiga mayowe, kutetemeka, kujikuna au kuwachuna wengine, kupata homa mara kwa mara bila sababu, maradhi ya kuzaliwa nayo, udhaifu wa mwili, kutokukua vizuri, kupungua kwa nyama ya mwili mpaka kuwa mwembamba sana, kuharisha kama maji, na kuwa na duara nyeusi chini ya macho; yote haya ni dalili za ugonjwa wa Umm-us-Sibyaan.
Kwa ajili ya kumlinda mtoto dhidi ya ugonjwa huu, hirizi(ta’wiz)
iliyopo katika kitabu iandikwe kwenye karatasi ya nta, ifunikwe vizuri na
kushonwa ndani ya kitambaa cha rangi ya samawati, kisha ivaliwe shingoni mwa
mtoto. Mara moja kwa wiki, hirizi(ta’wiz) ifukizwe ubani bila kuitoa ndani ya
kifuniko chake.