Topics

Athari Mbaya za Dawa au Sindano (Reaction)

 

Wakati mwingine matumizi ya dawa kali au zenye sumu huifanya damu kuwa na sumu.

Kutokana na hilo, vipele au madoadoa hujitokeza mwilini, na wakati mwingine mtu hupata mizinga.

Athari ikiwa kali zaidi, mgonjwa huhisi maumivu ya kuchoma kichwani na mwilini hupata degedege (spasms).

Wakati mwingine hupoteza fahamu.

Ikiwa damu imeathiriwa kutokana na Food Poisoning au kuumwa na viumbe wenye sumu kama nyoka, nge, nyigu au nyuki, soma Matendo ya Kiroho iliyotolewa katika kitabu na upulizie ndani ya maji.

Mnyweshe mgonjwa maji hayo.   


Pia pulizia kwenye kipande cha udongo laini na umnusishe mgonjwa mara kwa mara. 

Topics