Topics
Katika ugonjwa huu ndani ya kona ya jicho
hutokea chembe inayofanana na jipu dogo ambalo huendelea kutoa usaha. Hali hii
huitwa Nasoor ya Jicho.
Chukua punje moja ya choroko iliyogawanyika nusu
na jiwe.
Jiwe hilo liwe la aina inayopatikana kandokando
ya mito. Jiwe linaweza kuwa jeusi, jeupe, kahawia au lenye michoro na huwa
laini. Ukubwa wake hauna masharti.
Mimina maji juu ya jiwe na soma mara moja:
اَللّٰهُ نُوْرُ السَّمٰوَاتِ وَالْأَرْضِ
Allaahu Noorus-Samaawaati
Wal-Ardh
Kisha pulizia juu yake.
Sugua punje hiyo juu ya jiwe mpaka itengeneze
marhamu.
Marhamu hiyo ipakwe katika jicho lililoathirika
kwa kutumia sindano ya zinki asubuhi na jioni kwa siku kadhaa.